Share

Waziri wa Ujerumani Gerd Müller akutana na Rais Museveni

Share This:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa mchango wake mkubwa katika kushughulikia mzozo wa wakimbizi ambao unazidi kuwa changamoto kwa nchi hiyo.Waziri wa Ujerumani wa ushirikiano wa maendeleo Dr. Gerd Müller, amefafanua kuwa Ujerumani inazingatia pia mustakabali wa wakimbizi hao na ndiyo maana itawekeza zaidi katika kuwapa mafunzo ya ujuzi wa kiufundi ili waweze kujitegemea kwa sasa na baadaye.

Leave a Comment