Share

“Waziri yeyote akifanya jambo kafanya, sio lazima awe mwizi” – Spika Ndugai

Share This:

Spika wa Bunge Job Ndugai alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa hoteli ya Fantasy village iliyojengwa na Mbunge wa jimbo la Aman Mussa Hassan Mussa mkoani Dodoma.

Katika hotuba yake Spika alionesha kukerwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwasema vibaya wawekezaji Wazawa wa Tanzania na kuwaita Mafisadi.

“Sisi akiwekeza mzungu hatuna nongwa ila akiwekeza mswahili na bahati mbaya ni kiongozi ataitwa majina mengi yakiwemo fisadi, lazima tutoke huko… haiwezekani ” –Spika Job Ndugai

Leave a Comment