Share

Wenye matatizo ya kiakili, wanafungwa minyororo Ghana

Share This:

Nchini Ghana kuna madaktari wa afya ya kiakili 25 pekee wanaostahili kuhudumia takriban watu milioni 30.
Uhaba huu wa madaktari umesababisha jamaa za watu wenye matatizo ya kiakili, kuwategemea viongozi wa kidini. Hata hivyo viongozi hawa hawana ujuzi wa kitabibu na hivyo wanaishia kuwafunga minyororo ilikuwadhibiti wanaokisiwa kuwa ni ‘wenda wazimu’. Serikali iliharamisha tabia ya kuwafunga minyororo mwaka uliopita hata hivyo uchunguzi wa BBC umebaini kuwa sasa viongozi hao wa kidini wamewajengea vyumba vidogo kuwadhibiti.
Tazama ripoti hii kutoka Ghana, ya Sulley Lansah

Leave a Comment