Share

AVEVA NA KABURU WALIVYOPEWA DHAMANA

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.

Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 7 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamerudishwa mahabusu ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zachariah Hans Pope.

Kutokana na hatua hiyo washtakiwa hao wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni ka upande wa mashitaka, pia kwa kosa moja moja na sio kwa kutegemeana.

Leave a Comment