Share

Baada ya tiba ya saa 72 Kapombe imeshindikana kuitumikia Taifa Stars

Share This:

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo asubuhi ya July 18 2017 imefanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Taifa Stars ambayo itaondoka Mwanza July 19 kuelekea Kigali Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda, wachezaji wake wote wamefanya mazoezi ya pamoja kasoro beki Shomary Kapombe ambaye alikuwa akifanya mazoezi maalum na jopo la madaktari wa timu. Kama utakuwa unakumbuka vizuri Shomari Kapombe aliumia na kutolewa nje ya uwanja mapema katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda uliyomalizika kwa sare ya 1-1, AyoTV imempa daktari wa Taifa Stars Richard Yomba na kutaka kufahamu hali ya Shomari Kapombe.

Leave a Comment