Share

BIBI AHUKUMIWA MIAKA 99 JELA, SABABU YATAJWA

Share This:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 99 jela Salma Mntambo baada ya kupatikana na hatiani katika mashitaka 17 ikiwemo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Miaka hiyo 99 inatokana na makosa 14 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo kwa kila kosa amehukumiwa miaka sita jela, huku katika makosa matatu ya kutoa nyaraka za uongo kila kosa amehukumiwa miaka mitano jela.

Hata hivyo mshitakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka 6 jela kwa sababu miaka hiyo itaenda sambamba.

Hkumu hiyo, imetolewa na Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina ambapo amesema amepitia sababu za upande wa mashtaka na utetezi katika kesi hiyo, hivyo katika makosa matatu ya kutoa nyaraka za uongo mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kila kosa.

Pia katika makosa 14 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka sita jela kwa kila kosa.

“Huo ndio uamuzi wa mahakama lakini mna haki ya kukata rufaa, kuhusu suala la fidia nitatafakari na kufanya utafiti ili nije kutoa oda ambayo ni sahihi hivyo Oktoba 2, mwaka huu nitaitoa oda hiyo ya fidia, ” amesema Hakimu Mhina

Hata hivyo Hakimu Mhina aliamuru mshtakiwa huyo atumikie vifungo hivyo sambamba hivyo atakwenda jela miaka sita.

Leave a Comment