Share

DC CHUNYA: WAPELEKEENI SALAMU ZAO WANAONUNUA DHAHABU MAJUMBANI INAKUJA SIKU ISIYO NA JINA

Share This:

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi amepiga marufuku tabia ya watu binafsi kununua Dhahabu kutoka kwa wachimaji wadogo na badala yake ameagiza dhahabu yote inayopatikana iuzwe kwenye masoko madogo madogo ambayo yamefunguliwa kisheria wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea masoko ya Dhahabu ambayo yamefunguliwa kwenye migodi ya wachimbaji wadogo Wilayani Chunya ambako amegundua kuwa bado kuna Dhahabu ambayo inauzwa nje ya masoko hayo na ndipo akapiga marufuku tabia hiyo na kuonya kuwa yeyote atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Leave a Comment