Share

‘Hatujawashtaki DAWASA sababu Mahakama yetu ni Rais Magufuli’ -Diwani

Share This:

Leo March 19, 2018 Ninayo stori kutoka kwa Diwani wa CCM Kata ya Magomeni, Bujugo amesema hawajafungua kesi mahakamani kupinga kubomolewa nyumba zao na DAWASA kwa sababu Mahakama yao ni Rais John Magufuli.

Bujugo ameyasema hayo leo baada ya shirika la DAWASA kuweka alama ya X katika Kata 5 ikiwemo shule yake ya Green Acres ili kupisha ujenzi wa Bomba la Maji la Ruvu Juu.

Kata hizo ni Mbezi, Wazo, Bunju, Mbezi Juu, Mabwepande na Mbweni.

“Katika wiki hii ya Maji tunapongeza lakini imetuacha katika hali mbaya kwa sababu DAWASA wametuwekea alama ya kuvunja maeneo yetu kwa kutuwekea mita 15 kinyume na sheria,” -Bujugo.

Amesema kwa mujibu wa sheria ilipaswa wakae umbali wa mita lakini DAWASA wamewafanyia ukahidi na kuwataka wakae umbali wa mita 15.

“Tunamuomba Rais aingilie kati, bado hatujafungua kesi mahakamani kwa sababu mahakama yetu ni Rais John Magufuli,” -Bujugo

Amesema kuwa wanataka kufahamu DAWASA wanatumia sheria gani maana inaonekana kama wanataka kuwachonganisha wananchi na Rais John Magufuli.

Bujugo amemuomba Rais Magufuli asikilize kilio chao, kwa sababu DAWASA wamechokwa kwa tabia zao.

“Mimi ni muathirika nina shule yangu ya Green Acres ambapo ina wanafunzi zaidi ya 1000, pia nyumba ambazo zinaweza kuathirika ni zaidi ya 1000,”-Bujugo

Leave a Comment