Share

ISHU YA UHABA WA MAFUTA YAMUIBUA WAZIRI WA KILIMO “CHANZO NI CORONA”

Share This:

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amesema uhaba wa mafuta ya kula kwa sasa umesababishwa na changamoto ya ugonjwa wa Corona duniani.

Prof.Nkenda ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara kwenye baadhi ya viwanda vya kutengeneza mafuta ya kula vinavyotumia malighafi za kilimo kuyaandaa.

Katika hatua nyingine Prof.Nkenda amewataka wakulima kuhakikisha wanatumia hali hii ya uhaba wa mafuta kujikita katika kilimo cha mimea inayotoa bidhaa ya mafuta ya kula kwani kwa sasa Tanzania inazalisha asilimia 47 tu za mafuta wakati serikali inatumia nusu trilioni yakuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.

Katika hatua nyingine amesema serikali haijakataza kuuza mafuta ghafi nje ya nchi na kwa wale wayakaowazuia wawekezaji kiwekeza kwenye viwanda vya mafuta watachukulia hatua kali kisheria.

Leave a Comment