Share

Je raia wanaweza kulinda kura mara baada ya kupigaji kura?- Dira ya Dunia Ijumaa 16th Oktoba

Share This:

Tulionayo katika Dira ya Dunia Ijumaa 16th Oktoba
· Baada ya mgombea Urais wa Zanzibar, kupitia chama cha ACT Wazalendo kufungiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kufanya Kampeni, Maalim Seif asema hajui kosa lake.
· Leo ni siku ya chakula duniani huku mabadiliko ya tabia nchi, ni kati ya sababu zilizotajwa kusababisha upungufu wa uzalishaji wa chakula katika mataifa mengi duniani
· Wagombea wawili wa nafasi ya urais nchini Marekani wametoa tathmini zao za jinsi nchi hiyo inavyoshughulikia mgogoro wa Virusi vya corona
· Ofisi kuu ya takwimu nchini Kenya imedokeza kuwa uchumi wa nchi hiyo umezorota kwa kiwango kikubwa kutokana na makali ya janga la Covid 19.
· Na katika mjadala hii leo tunauliza, Je raia wanaweza kulinda kura mara baada ya shughuli ya upigaji kura?
Tuwe pamoja ifikapo hapo kumi na mbili unusu jioni , mimi ni Regina Mziwanda na mwenzangu ni Lynace Mwashighadi

#DirayaDunia
#MaalimseifShariff
#UchaguziTanzania2020

Leave a Comment