Share

MBUNGE WA VITI MAALUM WAFANYAKAZI JANEJELLY AANZA NA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Share This:

Mbunge wa Viti Maalum Wafanyakazi Mhe Janejelly James Ntate Ijumaa hii alitembelea hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanya kikao na Chama Cha Wafanyakazi wa hospitali hiyo kujua changamoto pamoja na kuangalia mazingira yao ya kazi.

Akizungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo aliwapongeza kwa kazi nzuri na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa Watanzania wanawategemea.

Amesema yeye ataendelea kuishauri serikali pamoja na CCM kutekeleza yale yote ambayo yaliahidiwa kwenye Ilani ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

Leave a Comment