Share

Mwanamke anayekula udongo kilo 20 kwa mwezi – katika Dira ya Dunia 15 Oktoba 2020

Share This:

 Jeshi la Nigeria limetoa onyo kwa watu wanaodaiwa kuwa mstari wa mbele kuzua vurugu, likiwakataka wakome…lakini mbona hali nchini humo bado ni tete?
 Wanafunzi wa mwaka wa mwisho nchini Uganda wamerudi shuleni miezi saba baada ya taasisi zote za elimu nchini humo kufungwa ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Hali imekuwaje?
 Huenda watu mashuhuri ikiwemo viongozi wa dini wakahusika kuleta maridhiano kwenye chama tawala cha Jubilee nchini Kenya.. Lakini je, upatanisho kati ya Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto utafaulu?
 Serikali ya Tanzania inasema itatumia helikopta na ndege kuzima moto ambao umekuwa ukiwaka Mlima Kilimajaro.
 Kutana na mwanadada ambaye si mjamzito lakini kwa wiki yeye hula hadi kilo nne za udongo ambazo ni sawa na kilo 20 kwa mwezi,
Ungana nami Phyllis Mwatee na Lynace Mwashighadi kuanzia kumi na mbili unusu jioni
#DirayaDunia
#MtKilimanjaro
#Udongo

Leave a Comment