Share

RC Makonda: Sijalala ile kauli ya Rais Magufuli / Ningejiuzulu / Mnenivua nguo

Share This:

Makonda aunda tume kushughulikia miradi ya kimkakati Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameunda tume itakayoongozwa na katibu tawala wa mkoa huo Abobakar Kunenge kushughulikia miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali kuu katika Mkoa wa Dar es salaam.

Makonda ametoa taarifa ya kuundwa kwa tume hiyo wakati akizungumza na watendaji na wazazi wa wanafunzi waliopatiwa ufadhili wa kusoma kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha tano waliofaulu masomo ya Sayansi kupitia mfuko aliouanzisha.

Mkuu wa Mkoa ameunda tume hiyo kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt John Magufuli ya kuwataka viongozi wa mkoa wa Dar es salaam kusimamia kwa ukaribu miradi inayotekelezwa na serikali katika mkoa huo.

Katika maelekezo hayo Mhe Rais kwanza alionesha kukerwa na ucheleweshwaji wa miradi ya Machinjio ya Kisasa eneo la vingunguti na mradi wa uboreshaji wa eneo la Coco Beach.

Baada ya maelekezo hayo Mkuu huyo wa Mkoa ametangaza kuunda tume itakayosimamia miradi mnne inayotekelezwa na serikali kuu katika mkoa wa Dar es salaam ambayo ni ujenzi wa soko la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Mbezi na Ujenzi wa Ufukwe wa Coco.

Leave a Comment