Share

USHIRIKIANO WA POLISI BURUNDI NA TANZANIA,WAKAMATA MAJAMBAZI SABA”WAKIPIGA WANAKIMBIA BURUNDI”

Share This:

Jeshi la polisi la nchi ya Burundi likishilikiana na jeshi la polisi la Mkoa wa Kigoma wamefanikiwa kuwakamata watu saba nchini Burundi wanaoshukiwa kuwa majambazi ambao wamekuwa wakitekeleza matukio ya uhalifu na ujambazi wa kutumia silaha Mkoani Kigoma.

Tukio hilo linathibitishwa na Msemaji wa jeshi la polisi nchini Burundi Meja Pierre Nkurikiyo mara baada ya kukutana na Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Martin Otieno mpakani mwa Tanzania na Burundi katika kjiji cha Mabamba wilayani kibondo mkoani humo.

Meja Nkurikiyo ameeleza kuwa baada ya mahojiano wamebaini kuwa majambazi hao wanatokea nchini Burundi ambapo wamekuwa wamekuwa wakienda katika makambi ya wakimbizi nchini Tanzania na kudai kuwa wao ni wakimbizi kisha kutekeleza matukio ya uhalifu na kukimbilia nchini Burundi.

Leave a Comment