Share

WABURUTWA MAHAKAMANI KWA KUCHAPISHA MAUDHUI MTANDAONI BILA LESENI “MWANAFUNZI WA CHUO”

Share This:

Vijana wawili wa Kitanzania wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kuchapisha maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Washitakiwa hao ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara CBE, Isaya Masawe (21) na Ofisa Habari Msaidizi wa CHADEMA, Dominic Mgaya ambao wamesomewa mashitaka kwa mahakimu wawili tofauti.

Wakili wa Serikali, Adolph Ulaya alidai kuwa kati ya February 4,2019 na Septemba 16,2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es salaam mshtakiwa huyo alichapisha maudhui mtandaoni kupitia channel ya YouTube Kwa jina la Isaya Thomas Masawe bila ya kupata leseni kutoka TCRA.

Leave a Comment