Share

WANAFUNZI RUKSA KUANZA SHULE BILA UNIFORM

Share This:

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ametoa maagizo kwa walimu kutowazuia wanafunzi wasiokuwa na vifaa vya shule kuanza masomo.

“Natoa agizo shule zote za Sekondari ndani ya wilaya yetu ya Kinondoni ni marufuku Mwanafunzi yoyote kunyimwa kupokelewa shuleni na kusajiliwa kuanza masomo kwa sababu ana ukosefu wa mahitaji fulani fulani, mahitaji ya msingi ni yeye kuripoti na kuwa na daftari, vifaa vya kujifunzia, sijui hana Jembe, hana uniform, hana viatu kisiwe kigezo.

Tumetoa ada ili watoto wa wanyonge kupata elimu, watoto wote kuanzia kiwango cha chini hadi wenye uwezo mkubwa tusiweke vigezo vya kuendelea kuwabagua, wapokelewe na wapewe Elimu,” amesema DC Chongolo.

Leave a Comment