Share

WANAKIJIJI”TOKA MWAKA 1970 WAZIRI YEYOTE HAJAWAHI FIKA KIJIJINI WAKWANZA KAWAWA,NDALICHAKO WAPILI”

Share This:

Waziri wa elimu sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi Prof Joyce Ndalichako ametoa mchango wa mabati 72 na mifuko 50 ya saruji kwajili ya ujenzi wa Kituo cha afya katika Kijiji cha Marumba kata ya Muhunga wilayani Kasulu Mkoani Kigoma jambo litakalowasaidia wakazi wa kijiji hicho kuacha kutembea umbali wa kilomita 50 kufuata huduma za afya .

Waziri Ndalichako ametoa mchango huo katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la mtakatifu Agustino kijijini hapo kanisa ambalo lilianzishwa tangu mwaka 1945 ambapo zaidi ya shilingi million 20 zilipatikana.

Aidha wakazi wa kijiji hicho wameeleza kuwa ni takribani miaka 70 sasa tangu hayati Waziri Rashidi Mfaume kawawa kufika kijiji hapo hakuna kiongozi yoyote mkubwa aliyewahi kufika ambapo waziri Ndalichako amewahidi kuwa kuanzia sasa viongozi mbalimbali wataanza kufika kijijini hapo.

Leave a Comment