Share

WANANCHI WAMSIMAMISHA SILINDE “WATOTO WETU WANASOMA CHINI YA MITI, NAWAPIGIA DC NA AFISA ELIMU”

Share This:

Wananchi wa kijiji cha Njinjo kata ya Njinjo wilaya kilwa mkoa wa lindi wameiomba serikali kuwasaidia ujenzi wa shule yao mpya ya msingi Njinjo ambayo wanafunzi wanasomea chini ya miti kama madarasa baada ya shule yao ya zamani kusombwa na mafuriko tarehe 25 january 2020 na kulazimika kuhama makazi yao ya zamani na kuhamia sehemu nyingine ambayo imewabidi wajenge shule mpya ili watoto wao waendelee kupata elimu.

Hayo wameyaeleza baada ya kusimamisha msafara wa Naibu wa Waziri wa TAMISEMI David Silinde aliyekua anapita njia kutoka kilwa kivinje kukagua miradi mbalimbali ya serikal akielekea Liwale na kumuomba aone jinsi wanafunzi hao wanavyosoma chini ya miti na kuwa mpaka sasa wamejitahidi kujenga madarasa matatu ambayo tayari wamekamilisha kuyajenga kwa nguvu za wananchi na fedha milioni 30 kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilwa na sasa wamepokea milioni 64 kutoka TAMISEMI ambayo wameambiwa wajenge madarasa matano ambayo wapo katika hatua ya uchimbaji wa msingi na kufyatua matofali.

Katika hatua nyingine wananchi hao wakiongozwa na Afisa mtendaji wa kata hiyo bi Pili Mgumba na Abuu Abdallah wamesema wanaumia kuona watoto wao wanasoma chini ya miti zaidi ya mwaka mzima huku walimu wa shule hiyo wakiwa hawana hata makazi wala ofisi ya walimu lakini hata vyoo ikiwa ni shida wakiwa wanatumia choo cha mda cha mabati chenye matundu matatu ambacho kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya 813 na walimu 9.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Njinjo Mabruki Jaffari amesema shule hiyo ilianza mwaka 1945 enzi za ukoloni na baadae mwaka mmoja uliopita ilisombwa na mafuriko na kufanya waanze kujenga upya madarasa eneo jengine salama na kwasasa inaupungufu wa madarasa 15 na matundu ya vyoo 36,ofisi ya walimu na mwalimu mkuu,matundu ya choo ya walimu makazi ya walimu na stoo ya vitabu hali inayopelekea utoaji wa elimu kua ni shida kwani kwasasa wanafunzi wa darasa la awali,tatu,tano na sita bado wanasomea chini ya miti huku darasa la saba,nne na kwanza na pili wakiwa katika madarasa yaliyo kamilika .

Akijibu kero hizo Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amesema ofisi yake imeleta milioni 62 wajenge madarasa na mwenye jukumu la kusimamia hizo fedha ni yeye na kuwataka wazitumie fedha hizo kujenga wakishakamilisha majengo wamdai madarasa mengine matatu na kuwataka waongeze kasi ya ujenzi ili wayapate madarasa mengine mapya haraka.

“Nimelizishwa na wananchi wanavyojitolea katika ujenzi wa madarasa,namabiwaa hapa chini ya miti ndio madarasa hata mimi sijafurahishwa madarasa kuchelewa mwaka mzima bila kujengwa nikitoka hapa nampigia simu mkuu wa wilaya na afisa elimu waniandikie maelezo kwanini wameshindwa kukamilisha madarasa watoto wakae, nataka ndani ya miezi miwili madarasa haya yawe yamekwisha na watoto wote hakuna kusoma chini tena” Naibu waziri Silinde.

Kabla ya kufika shuleni hapo Naibu Waziri Silinde alifanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa lipa kwa matokeo EP4R katika shule za Ming’umbi Sekondari na Kivinje Sekondari na kuridhika na ujenzi wa madarasa na kutaka wakamelisha yote kwa asilimia 100 huku akitaka wakurugenzi kuanza kujipanga ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kutumia fedha za ndani kwani hawataki kusikia mwakani kuna shida ya madarasa nchini.

Leave a Comment